Taarifa kutoka nchini Ujerumani na England zinadai kwamba klabu za Bayern Munich na Manchester City zipo kwenye mazungumzo ya mwisho kwa ajili ya kufanikisha usajili wa winga wa Manchester City na timu ya taifa ya Ujerumani, Leroy Sane.
Ripoti zinadai kwamba jambo hilo lipo kwenye hatua za mwisho kabisa kumalizika na pindi litakapoibuka tena litakuwa ni suala la kutangazwa rasmi kwa mchezaji huyo kuwa mchezaji wa Bayern Munich.
Kwa sasa ligi zote nchini zimesimamishwa kutokana na janga la Virusi vya Corona vilivyoikumba dunia ila serikali imetangaza kuwa kuna uwezekano wa ligi kurejea mwezi Juni.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.