David Kameta ‘Duchu’ ametambulishwa rasmi leo Agosti 15 ndani ya kikosi cha Simba akiwa amesaini dili la miaka miwili akitokea klabu ya Lipuli Fc.
Duchu akiwa Lipuli ambayo itashiriki ligi daraja la kwanza msimu ujao alitupia mabao matatu na kutoa jumla ya pasi saba kwa msimu wa 2019/20.
Simba Sc inazidi kukisuka vyema kikosi chao kwa ajili ya msimu wa 2020/2021 licha ya kuwa wametwaa taji la ubingwa kwa msimu uliopita na Kombe la Shirikisho (ASFC).
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.