Uwanja wa Taifa wa Kasarani uliopo jijini Nairobii nchini Kenya umechaguliwa kuwa uwanja utakaofanyika mchezo wa fainali wa Kombe la Mataifa ya Afrika (CHAN) 2024, ambalo linafanyika nchini Kenya,Tanzania na Uganda.
Mchezo huo utachezwa Jumamosi Agosti 30, na unatarajiwa kuwa na mvuto kwa kiwango cha juu baada ya mashindano hayo ya miezi miwili yanayotarajiwa kuvutia mashabiki wa soka katika nchi zote tatu za Afrika Mashariki.
Kamati ya Maandalizi ya Local Organizing Committee (LOC) ilithibitisha kuwa uwanja huo, uliopo Nairobi, utakuwa ndio wa mwisho kwa michuano hiyo baada ya kukamilika kwa matengenezo yake.
“Tumalizika kwa uboreshaji wa Kasarani kunaleta fursa kwamba sasa tunaweza kutumia uwanja huo kwa mchezo wa fainali,” alisema Mwenyekiti wa LOC, Maurice Amollo.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Uwanja wa Kasarani pia utatumika kwa michezo mingine muhimu, ikiwa ni pamoja na mechi ya kufungua mashindano na nyingine za hatua ya makundi ambapo kundi A lenye timu za Kenya,Morocco,Angola,Dr Congo na Zambia.
Mechi nyingine za mashindano zitachezwa katika uwanja wa Moi International Sports Centre, Kasarani, na uwanja wa Kinoru huko Meru.
Huu utakuwa mara ya kwanza Kenya kukumbwa na mashindano ya CHAN, ambayo ni ya timu za taifa zenye wachezaji wanayocheza katika ligi za nyumbani.