Mshambuliaji aliyekuwa anakipga ndani ya CD Tennerife ya Hispania,Farid Mussa ametangazwa rasmi leo kuwa mali ya Yanga baada ya kumwaga wino wa kuitumikia klabu hiyo kwa dili la miaka miwili.
Mussa ameibukia ndani ya Yanga akiwa ni mchezaji huru baada ya dili lake la miaka minne ndani ya CD Tennerife kuisha na amekuja kuziba nafasi ya mnyarwanda,Sibomana ambaye alisitishiwa mkataba na yanga baada ya msimu wa 2019/2020 kumalizika.
Mkataba huo umesainiwa mbele ya mkurugenzi wa uwekezaji wa GSM,Mhandisi Hersi Said ambao mbali na kuidhamini klabu hiyo pia imeamua kusimamia usajili ili kukiboresha kikosi cha yanga katika msimu ujao wa 2020/2021.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.