Kocha mkuu wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer ameonekana akimpigia hesabu mchezaji wa Sporting Lisbon Bruno Fernandes baada ya usajili wa dirisha dogo kufunguliwa mwezi Januari.
Bruno Fernandes anatajwa na kocha huyo kuwa mbadala wa kiungo wake Paul Pogba ambaye anasumbuliwa na majeraha kwa sasa.
Ugumu unakuja kwa Manchester United kumpata nyota huyo kwani watani wao Manchester City na Chelsea wanatajwa kuwania saini ya mchezaji huyo.