Wadhamini wa klabu ya Yanga sc kampuni ya GSM imesema kuwa mwanachama na mwenyekiti wa zamani wa klanu hiyo Yusufu Manji yupo huru kununua hisa za timu hiyo.
Hayo yameelezwa na mkurugenzi wa uwekezaji GSM Injinia Hersi alipokuwa katika mahojiano maalumu na kituo cha azam media.
Hersi alisema kuwa ”Manji anakaribishwa kununua hisa za klabu hiyo kwasababu mfumo wa umiliki wa hisa wa klabu ya Yanga si wa mtu mmoja, bali unaruhusu wawekezaji zaidi ya watatu”.
Hilo limekuja mara baada ya kurejea kwa Manji kwenye mkutano mkuu wa mabadiliko wa klabu hiyo na kupelekea kushangiliwa kwa nguvu na wanachama wa Yanga hali iliyozua sintofahamu juu ya hatima ya GSM ambao wamekua mstari wa mbele kuipeleka Yanga kwenye mabadiliko.