Simba Sc leo imeibuka na ushindi wa mabao 6-0 mbele ya AFC leo kwenye mchezo wa kirafiki uliochezwa uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.
Bao la kwanza na la tatu lilipachikwa na Meddie Kagere dakika ya 4 na 34 huku bao la pili lilifungwa na Larry Bwalya dakika ya 24.
Kipindi cha pili cha mchezo Simba Sc ilipachika mabao mengine matatu kupitia Luis Miqussone ambapo walifikisha idadi ya mabao 6-0 na kuwamaliza nguvu wapinzani wa AFC.
Simba wanajiandaa na mchezo wa ligi kuu bara dhidi ya Ihefu unaotarajiwa kuchezwa Septemba 6 uwanja wa Sokoine na AFC wao wanajiandaa na ligi daraja la kwanza.