Bodi ya ligi kuu ya Tanzania imetangaza kuwa vilabu vyote vinavyoshiriki ligi hiyo vimekubaliana kwa pamoja kuwa hakutakuwa na mechi itakayokuwa inachezwa pindi wawakilishi wa nchi katika mashindano mbalimbali ya kimataifa watakapokuwa wanacheza,hivyo ligi itakuwa inasimama kila kipindi hicho kikifika.
Hatua imekuja kuondoa tatizo la wingi wa mechi za viporo pindi timu za ndani zinapokuwa zinashiriki michuano mbalimbali ya CAF.
Mtendaji mkuu wa bodi ya ligi amesema kuwa wamefanya hivyo ili kumaliza changamoto ya mechi za viporo,hivyo hatua hiyo itaondoa kabisa na hakutakuwa tena viporo kwenye ligi hiyo.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.