Mbwana Samatta ambaye hivi leo amekamilisha usajili wake wa kusaini mkataba wa miaka minne na nusu ndani ya Aston Villa ana hatihati kubwa ya kuukosa mchezo wa leo dhidi ya Watford.
Mchezaji huyo amekuwa akizungumziwa sana kabla ya usajili wake kukamilika na imemchukua kipindi kirefu hadi hivi leo kuukamilisha na kuwa miongoni mwa Aston Villa timu ambayo inashiriki ligi kuu Uingereza.
Aston Villa hivi leo itawakaribisha Watford katika uwanja wake wa nyumbani katika mchezo wa ligi kuu nchini Uingereza ikiwa ni siku ya kwanza Mbwana Samatta kuwa miongoni mwao.
Hii inaleta uwezekano mkubwa kwa mchezaji huyo kutoshiiki mechi ya leo kwani mpaka sasa hajatambulishwa rasmi kwa wachezaji wenzake na pia hajauzoea bado uwanja wa Villa.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.