Home Makala “Hatuna Presha”Gamondi

“Hatuna Presha”Gamondi

by Dennis Msotwa
0 comments

Kocha mkuu wa klabu ya Yanga sc Miguel Gamondi amesema kuwa hana presha yeyote kuelekea mchezo wa fainali ya ngao ya jamii dhidi ya Yanga sc kwa kuwa kikosi chake kina maandalizi ya kutosha na hii sio derby yake ya kwanza kuicheza.

Gamondi ambaye ni raia wa Argentina amesema hayo mapema wakati wa mkutano na waandishi wa habari kuelekea mchezo wa ngao ya jamii utakaofanyika katika uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.

“ Ni Furaha kwangu kucheza mchezo huu mkubwa kesho, matarajio yetu ni kufanya vizuri na tumejiandaa bila presha yoyote kwasababu nimeshakutana na michezo ya aina hii mingi, tunaenda kupambana kwa ajili ya nembo ya Young Africans SC na Mashabiki wetu ambao wapo nasi kiła siku, ”

banner

“ Utakuwa mchezo mkubwa na mzuri kwetu hasa kwa mwanzo wa msimu na najua umuhimu wa mchezo huu kwa kila mmoja wetu, ”Alisema Gamondi

Yanga sc itakua na wakati mgumu kupata matokeo katika mchezo huo ikizingatiwa kuwa Simba sc haitokubali kukosa taji hilo kwa mara ya tatu mfululizo baada ya kulikosa misimu miwili iliyopita.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited