Uongozi wa klabu ya Jkt Tanzania leo Machi 18,2020 umevunja kambi yake kutokana na maelekezo yaliyotolewa jana na Serikali kupitia kwa waziri mkuu Kasim Majaliwa kuhusu zuio la kuwepo kwa mikusanyiko mbalimbali kutokana na kuwepo ugonjwa wa Virusi vya Corona hapa nchini.
Taarifa iliyotolewa na ofisa habari wa Jkt Tanzania , Jamila Mutabazi imeeleza kuwa wachezaji wote wanarejea nyumbani kuanzia leo.
Wachezaji wote wametakiwa kuendelea kujikinga na kufuata maelekezo yanayotolewa na Serikali sambamba na wataalam wa afya ili kuweza kupambana na virusi hivyo vya Corona.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.