Nyota wa zamani wa Manchester United,Psg na Ac Milan Zlatan Ibrahimovic yupo nchini Tanzania kwa ajili ya kutembelea vivutio mbalimbali vya utalii vinavyopatiakana hapa nchini.
Zlatan amechapisha picha kwenye ukurasa wake wa mtandao wa Instagram akiwa eneo la Kogatende kwenye hifadhi ya Taifa ya Serengeti nchini Tanzania eneo ambalo ni kitovu cha uhamaji wa wanyama maelfu wanaovuka Mto Mara kueleka nchini Kenya ama kuja nchini.
Inafahamika kwamba mwezi huu wa juni ndio msafara huo wa wanyama hasa nyumbu huvuka mto Mara kwa ajili ya kutafuta malisho tukio ambalo huwa ni la kiekolojia zaidi na huvutia watalii wengi duniani.
Zlatan (43) raia wa Sweden ambaye amewahi pia kuichezea Ajax, PSG, AC Milan na Barcelona ambaye kwa sasa ni sehemu ya washauri wa klabu ya AC Milan yupo Tanzania kwa ajili ya mapumziko ya mwisho ya msimu.