Uongozi wa KMC umethibitisha kuwa Charlse Ilanfya ni mali rasmi ya Simba Sc kwani ndio klabu pekee iliyopeleka ofa ya kupata saini ya mshambuliaji huyo.
Ilanfya aliibukia ndani ya KMC akitokea klabu ya Mwadui Fc amekuwa kwenye msimu mzuri kwenye mechi za mwisho za KMC kwa kuwa awali alikuwa akisumbuliwa na mejeraha ya misuli ya nyama za paja.
Ilanfya ametupia jumla ya mabao sita akiwa ya KMC kwenye ligi kuu bara jambo lililowavutia Simba kuongeza nguvu ndani ya kikosi hicho ambacho kina taji la Ligi Kuu Bara kwa msimu wa 2019/20 na kitaiwakilisha nchi kwenye mashindano ya kimataifa.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.