Home Makala Injinia Apora Kiungo Tp Mazembe

Injinia Apora Kiungo Tp Mazembe

by Sports Leo
0 comments

Baada ya Eng Hersi Said kukamilisha dili la Djuma Shabani, taarifa za kuaminika kutoka nchini Congo zinasema kuwa pia bosi huyo amekamilisha dili la nahodha wa klabu ya Maniema Union, kiungo fundi Mercey Vumbi Ngimbi na anatarajiwa kujiunga na klabu ya Yanga muda wowote kwani kila kitu kimekamilika.
Ngimbi amerejea jana nchini Congo na tayari ameshawaambia mabosi wa Maniema Union kwamba anataka kwenda Yanga aungane na Tuisila Kisinda, Mukoko na Djuma Shabani huku Msimu huu ameisaidia timu yake kumaliza katika nafasi ya 3 nyuma ya TP Mazembe kwenye Ligi Kuu ya Congo huku yeye pekee akifunga mabao 7 na kutoa assists 9.
Taarifa zaidi zinadai kwamba mchezaji huyo alikua mbioni kujiunga na Tp Mazembe lakini kuingia kwa Yanga sc kwenye dili hilo kumemfanya atamani kuja Tanzania huku mkataba wa muda mfupi anaopewa na Yanga sc ndio unamvuta zaidi ili kurahisisha dili la kucheza nje ya nchi.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited