Home Makala Inonga Nje Wiki Mbili

Inonga Nje Wiki Mbili

by Sports Leo
0 comments

Beki wa kati wa Simba, Henock Inonga atakuwa nje ya Uwanja kwa wiki mbili kuuguza jeraha la bega alilopata kwenye mchezo wa nusu fainali ya Ngao ya Jamii dhidi ya Singida Fountain Gate Fc.

Inonga alipata jeraha hilo la bega dakika za mwishoni mwa mchezo huo ambao Simba sc walishinda kwa matuta na kufanikiwa kuingia fainali ambapo walicheza na Yanga sc na kufanikiwa kuibuka na ushindi wa 3-1 kwa matuta ambapo beki huyo alikua jukwaani kutokana na maumivu hayo.

Inonga msimu tayari alishatengeneza pacha nzuri kati yake na beki mpya Che Malone Fondoh wakianza katika michezo miwili msimu huu ule wa Simba day dhidi ya Power Dynamos ya Zambia na ule dhidi ya Singida Fountain Gate ambao pia waliibuka na ushindi huku wakiwa hawajaruhusu goli la kufungwa.

banner

Beki Kennedy Juma ataendelea kuishikilia nafasi hiyo kwa muda mpaka pale Inonga atakaporejea baada ya hizo wiki mbili.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited