Aliyekuwa kiungo fundi wa zamani wa timu ya Simba Sc ambaye kwa sasa anakipiga katika klabu ya Kaizer Chiefs James Kotei anatarajia kutua Yanga kwa mkopo.
Yanga ilikuwa na mpango wa kumnasa kiungo mkabaji kutoka Zesco Utd Anthony Akum raia wa Kenya kumbe Kaizer Chiefs nao walikuwa na mpango wa kumnasa mchezaji huyo.
Kutokana na ukaribu walionao Yanga na Kaizer wamefanya kubadilishana James Kotei atue Jangwani na Akum aende Kaizer Chief.
Taarifa zaidi zinadai dili hilo linaweza kukamilika kabla ya dirisha la usajili kufungwa siku ya jumatano wiki ijayo.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.