Home Makala Juve Wamvizia De gea

Juve Wamvizia De gea

by Dennis Msotwa
0 comments

Wazee wa mterezo, Juventus Fc wameanza kuivizia saini ya kipa wa timu ya taifa ya Hispania na Manchester united David De gea baada ya mchezaji huyo kugoma kusaini mkataba mpya baada ya ule wa awali kufikia tamati mwaka 2020.

De gea alijiunga na Manchester united june 2011 kipindi cha Sir Alex Ferguson na amekua kipa namba moja katika klabu hiyo kwa muda wote na kufanikiwa pia kupata nafasi katika timu ya taifa ya hispania na licha ya kuwekewa mshahara wa paundi 350000 kwa wiki kipa huyo amegoma kusaini mkataba mpya.

Kipengele cha kukata 25% baada ya timu kushindwa kufuzu michuano ya klabu bingwa barani ulaya kinatajwa kuwa ni chanzo cha mastaa wengi kugoma kuongeza mikataba klabuni hapo kutokana na kutoona dalili za timu hiyo kufanya vizuri kutokana na usajili unaosuasua.

banner

Juventus ni mabingwa wa kusajili wachezaji ambao mikataba yao imefika tamati wakifanya hivyo kwa Emre can,Sami Khedira,Aaron Ramsey na Buffon na hivi sasa wamehamishia karata ya jijini Manchester.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited