Nchini Italia nyota wa Juventus na timu ya taifa ya Ufaransa ,Blaise Matuidi amegundulika kuwa ana virusi vya Corona baada ya kufanyiwa vipimo.
Mwanasoka huyu amekuwa mchezaji wa pili Juventus kukutwa na maambukizi ya virusi vya Corona baada ya beki ,Daniele Rugani.
Matuindi ametengwa kwa hiari nyumbani kwake tangu Jumatano na ataendelea kufuatiliwa kwa kufuata utaratibu wa serikali japo kwa sasa anaendelea vizuri chini ya uangalizi maalum.