Home Makala Kagere Aizamisha Mtibwa Sugar

Kagere Aizamisha Mtibwa Sugar

by Sports Leo
0 comments

Bao la jioni la mshambuliaji wa zamani wa Simba sc Meddie Kagere limaizamisha klabu ya Mtibwa Sugar na kuwanyima alama tatu katika mchezo wa ligi kuu uliofanyika katika uwanja wa Liti mjini Singida.

Awali mapema dakika ya 12 ya mchezo huo faulo iliyopigwa na Rodyrigo iliweza kuzama moja kwa moja nyavuni na kuandikia Singida Big Stars goli la kwanza na mapema mwishoni mwa kipindi cha kwanza Meddie Kagere aliipatia uhakika wa kuchukua alama tatu Singida Big Stars kwa kufunga bao la pili.

Mtibwa Sugar licha ya kujalibu kujitutumua ilijikuta inatoka bila alama baada ya dakika tisini za mchezo huo mkali na wa kusisimu hasa katika kipindi hiki cha lala salama.

banner

Kutokana na ushindi huo Singida Big Stars imesalia katika nafasi yake ya nne ikiwa na alama 47 huku Mtibwa Sugar ikiwa katika nafasi ya tisa ya msimamo wa ligi kuu ya Nbc ikiwa na alama 29 zote zikiwa zimecheza michezo 24.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited