Beki wa klabu ya Simba sc Shomari Kapombe pamoja na winga Peter Banda wataukosa mchezo wa marudiano dhidi ya Premero De Augosto ya nchini Angola utakaofanyika katika uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar es salaam siku ya Jumamosi.
Katika mchezo wa awali Simba sc ilifanikiwa kupata ushindi wa mabao 3-1 nchini Angola ambapo mastaa hao walikua na majeraha na kuukosa mchezo huo ambapo hivi sasa wapo katika hatua za mwisho za kupona baada ya kuanza mazoezi mepesi mepesi lakini wanakosa utimamu wa mwili kwa ajili ya mchezo huo.
Simba sc itakua na kazi rahisi ya kulinda ushindi huo wa ugenini ili kujihakikishia nafasi ya kushiriki katika hatua ya makundi ya michuano hiyo mikubwa barani Afrika ambapo wamefika mara kadhaa huku wakiishia hatua ya robo fainali ya michuano hiyo.
Tayari mashabiki wa klabu hiyo wameshaanza kununua tiketi kwa ajili ya mchezo huo ambao unatarajiwa kujaza mashabiki wengi zaidi nchini katika michezo ya kimataifa kutokana na kuongezeka kwa kiwango cha klabu hiyo uwanjani katika michezo ya hivi karibuni.