Rais wa Shirikisho la soka nchini Tanzania Wallace Karia amechaguliwa kuwa mjumbe wa kamati ya utendaji ya shirikisho la soka barani Afrika(CAF) itakayokua inaongozwa na Rais wa Shirikisho hilo Patrice Motsepe.
Karia amechaguliwa kama mjumbe mwakilishi kutoka upande wa Shrikisho la soka ukanda wa Afrika Mashariki na kati (Cecafa) ambapo pia anaungana na wajumbe wengine wakiwamo Samuel Etoo kutoka ukanda wa Uniffac,Said Walid kutoka ukanda wa Unaf,Mustapha Ishola kutoka ukanda wa Wafu Pamoja na Kurt Edwin kutoka ukanda wa Wafu B Pamoja na bibie Bestine Kazadi.
Katika mkutano huo wa kuchagua wajumbe watakaoingia katika mkutano mkuu wa Caf ambao pia ulimchagua Motsepe kuendelea kuliongoza shirikisho hilo kwa kipindi kingine cha miaka minne baada ya kuchaguliwa kwa mara ya kwanza mwaka 2021.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Motsepe amechaguliwa kwa mara ya pili bila kupingwa katika uchaguzi ulioshuhudiwa na Rais wa Shirikisho la soka duniani (Fifa) Gian Infantino uliofanyika machi 11 jijini Cairo huku wadau wengine wa michezo nchini Kama Eng.Hersi Said,Salim Abdallah na Wilfred Kidao wakihudhuria.