Siku chache baada ya kuachana na Ihefu Sc Zuberi Katwila ameonekana akishirikiana na makocha wengine wa timu ya Taifa ya wanaume U15 katika kituo Cha ufundi Cha TFF, Mnyanjani, Tanga katika maandalizi ya mashindano ya CECAFA.
Ingawa haijafahamika bado kuhusu hatma yake baada ya kuchana na timu hiyo yenye makao yake Mbarali mkoani Mbeya tangu aachane nao rasmi siku ya Jumamosi huku pia kukiwa na taarifa za kujiunga na Singida Fountain Gate kama kocha msaidizi ama kurudi klabu yake ya zamani ya Mtibwa Sugar.
Katwila ameonekana kupitia video fupi iliyowekwa na mtandao wa kijamii wa shirikisho hilo inayoonekana hapo chini.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Awali Katwila baada ya kuachana na Ihefu alisema kuwa mpaka sasa bado hajapata timu “Sijafanya mazungumzo na timu yoyote ila itakayokuwa tayari kunihitaji tukakubaliana mimi niko tayari hata Ihefu naweza kurudi kwa sababu sijaondoka kwa ubaya zaidi ya makubaliano,” Alisema Katwila
Kocha huyo alidumu klabuni hapo kwa miaka mitatu tangu alipojiunga na timu hiyo akitokea Mtibwa Sugar.