Kocha mkuu wa Mtibwa Sugar ,Zuberi Katwila ameahidi kurudi kwa kasi na kutoa ushindi wa hali ya juu pindi ligi kuu bara itakaporejea baada ya kusimamishwa na serikali ili kupambana na mlipuko wa virusi vya Corona.
Katwila alisema kuwa anatafuta mbinu mbadala ya kuitoa Mtibwa katika nafasi ya 14 iliyo na pointi 33 huku ikiwa imecheza mechi 29 pia kuwataka wachezaji wake kuzingatia mazoezi kama walivyokuwa kambini ili kuboresha uwezo wao.
“Ligi ikianza nitarudi kwa kasi kuhakikisha wachezaji wanabadilisha timu irudishe hadhi Morogoro”alisema kocha huyo aliyewahi kuichezea timu hiyo kwa mafanikio makubwa.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Pia Katwila aliwasisitiza wachezaji wake watumie muda huu vizuri kwa kufuata maelekezo ili waweze kufikia malengo.