Nyota wa Aalborg BK ya Denmark Kelvin John tayari amejiunga na kambi ya timu ya Taifa ya Tanzania ambayo imekita kambi ya maandalizi kujiandaa na mchezo wa kufuzu kombe la Dunia dhidi ya Morocco.
Taifa stars imeweka kambi mkoani Tanga ambapo wachezaji na maafisa wengine wa timu wanakaa katika hoteli ya Tanga Beach Resort na wamekuwa wakifanya mazoezi Uwanja wa Mkwakwani.
Mshambuliaji huyo ni moja ya washambuliaji wa kati wanaotegemewa kuongoza safu ya ushambuliaji ya timu hiyo katika mchezo huo mkali haswa baada ya mshambuliaji Mbwana Samata kutoitwa kutokana na kuwa na majeraha.
Stars inatarajiwa kusafiri mchana wa leo kuelekea nchini humo kupitia Kilimanjaro ikitokea moja kwa moja jijini Tanga ilipokua imeweka kambi ya maandalizi.