Klabu ya Kengold Fc imejikuta ikiambulia kichapo cha mabao 5-0 kutoka kwa Simba sc licha ya kuwa nyumbani katika uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mkoani Tabora.
Katika mchezo huo ambao nusra Kengold Fc wasitokee uwanjani baada ya kuripotiwa kuwa wachezaji wamegoma wakishinikiza malipo ya mishahara wanayodai kwa miezi miwili mpaka sasa.
Mabao ya Simba Sc yalipatikana kuanzia dakika za 20 likifungwa na Kibu Dennis huku dakika sita baadae alifunga bao la pili na Ellie Mpanzu alifunga bao la tatu 32 huku Lionel Ateba na Jean Charles Ahoua walihitimisha ushindi wa mabao 5-1.
Kutokana na ushindi hu Simba Sc imeendelea kuibana Yanga sc katika msimamo wa ligi kuu ya ambapo tofauti yao ni alama moja.