Salum Kihimbwa ameibuka shujaa wa mchezo kati ya Kmc na Mtibwa Sugar baada ya kufunga bao pekee katika mchezo huo lililopeleka ushindi katika klabu hiyo ya Manungu mjini Morogoro.
Bao hili lilitokana na uzembe wa mabeki na kipa Juma Kaseja ambapo baada ya kupigwa krosi mfungaji alipiga kichwa akiwa katikati ya mabeki wa timu hiyo huku kipa Juma Kaseja akiwa kaliacha goli bila uhakika wa kuucheza mpira.
Licha ya juhudi za washambuliaji Emmanuel Mvuyekure na Reliants Lusajo mchezo ulibaki kuwa mgumu kwa Kmc iliyopoteza alama tatu.