Home Makala Kipa Rivers Ajipeleka Azam Fc

Kipa Rivers Ajipeleka Azam Fc

by Sports Leo
0 comments

Kipa wa klabu ya Rivers United ya nchini Nigeria Victor Sochima amevutiwa na ligi ya bongo huku akithibitisha kutamani kuichezea Azam Fc ambayo inasifika kwa kulipa mishahara minono mastaa wa timu hiyo.

Kipa huyo aliyecheza michezo yote miwili ambayo walifungwa na Yanga sc nchini Nigeria 2-0 na ule wa suluhu uliofanyika hapa nchini katika uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar es salaam.

Kipa huyo amethibitisha kuwa baadhi ya timu  zilimfuata kuzungumza naye ingawa kwa sasa akili yake ameiwekeza kwa ajili ya kuhakikisha msimu huu unaisha.

banner

“Siwezi kuweka wazi kwenye kila kitu kinachoendelea lakini itoshe kusema ni kweli nimefuatwa na baadhi ya timu ikiwemo Yanga kwa sababu baada ya mechi yetu kuisha nilifuatwa na kocha wao, Nasreddine Nabi alinifata tukazungumza baada ya mchezo kuisha”.

Hata hivyo pamoja na Yanga sc kumuulizia kipa huyo,yeye mwenyewe ameonyeshwa kuvutiwa zaidi na kujiunga na klabu ya AzamFc.

“Pale Azam kuna rafiki yangu mkubwa anaitwa, Isah (Ndala) ni mchezaji mzuri ambaye nimekuwa naye kwa ukaribu hivyo nitafurahia kama itatokea siku moja tutacheza wote pamoja ingawa kwa sasa dili bado halijakamilika.”

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited