Home Makala Kipa Simba sc Aula

Kipa Simba sc Aula

by Sports Leo
0 comments

Mambo yamemnyookea kipa namba tatu wa klabu ya Simba sc Ally Salim baada ya mabosi wa klabu hiyo kukubali kumpa mkataba wa miaka mitatu ukiwa na thamani ya Shilingi milioni 30 na mshahara wa milioni nne kwa mwezi.

Awali inasemekana kuwa kipa huyo alikua akilipwa nusu ya mshahara huo mpya lakini sasa kutokana na kuonyesha kiwango kizuri katika mchezo dhidi ya mahasimu Yanga sc na kuibuka na ushindi wa 2-0 mchezo uliofanyika katika uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar es salaam.

Taarifa za ndani kutoka klabuni hapo ni kwamba awali mabosi wa klabu hiyo walipanga kumtoa kwa mkopo kipa huyo lakini hivi sasa baada ya kuonyesha kiwango kizuri katika michezo miwili na kutokua fiti kwa kipa Aishi Manula huku Beno Kakolanya akiwa katika harakati za kujiunga na Singida Big Stars uongozi ukaona ni vyema umpe mkataba mpya huku kukiwa na uwezekano kukaa langoni tena dhidi ya Wydad Athletic Club siku ya kesho.

banner

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited