Kiungo wa Yanga Sc ,Haruna Niyonzima amelazimika kuwavuta karibu kwenye mazoezi ya pamoja wakongwe wenzake ,Juma Kaseja na Shabani Kado ikiwa ni mikakati mahususi ya kujiandaa na tamko la shirikisho la soka Tanzania(TFF)la kurejea kwa ligi kuu Bara.
Awali nyota huyo alikwa akifanya mazoezi mara moja kwa siku nyumbani kwake baada ya ligi kusimamishwa,lakini kwa sasa ameamua kuungana na kaseja pamoja na Kado ambapo wanafanya mazoezi hayo mara mbili kwa siku katika ufukwe wa Escape One ,Mikocheni.
“Nilikuwa nafanya kweli mazoezi mara moja tena nyumbani maana kuna nafasi ya kutosha ambayo ilikuwa inaniwezesha kwenda na program za kocha,ila kadri siku zinavyoenda nimelazimika kuongeza muda wa mazoezi ambapo sasa hivi nafanya na Kaseja pamoja na Kado”