Viongozi wa klabu ya Simba wamewaahidi wachezaji kuwapa kitita Cha Shilling milioni 200 kama watapata alama tatu kwenye mchezo wa mzunguko wa Tano wa kundi C katika michuano ya klabu bingwa barani Afrika dhidi ya Horoya,
Ikumbukwe kuwa mchezo huo utapigwa siku ya Jumamosi ya wiki hii katika uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam majira ya saa Moja kamili usiku ambapo endapo Simba sc itawafungwa Horoya Fc basi itakua na uhakika wa kwenda robo fainali kama mshindi wa pili wa kundi C nyuma ya Raja Casablanca.
Msimamo wa kundi hilo mpaka sasa ni Simba sc wapo nafasi ya pili wakiwa na alama sita huku Raja Casablanca wakiwa kileleni na alama 12 na Horoya Fc wakiwa nafasi ya tatu na alama nne huku Vipers Fc wakishika mkia na endapo Simba sc atafanikiwa kuwafunga basi atafikisha alama tisa ambazo haziwezi kufikiwa na Horoya wala Vipers.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.