Klabu ya Yanga sc imekwama katika mpango wake wa kumtumia Tuisila Kisinda katika kikosi cha timu hiyo katika mashindano ya ndani na nje ya nchi baada ya Shirikisho la soka nchini kuzuia usajili wake wakisema tayari klabu hiyo ilishakamilisha usajili wa wachezaji wa kigeni katika mfumo wa usajili wa Fifa.
Yanga sc ilimsajili Kisinda dakika za mwisho huku ikimuondoa Lazarus Kambole katika orodha ya wachezaji wake baada ya kuumia katika mchezo wa kirafiki hivyo kuhitaji muda mrefu zaidi wa matibabu na kuilazimisha klabu kuchukua maamuzi hayo.
Taarifa zilizosambaa hivi leo na kuwa gumzo kwa wadau wa soka nchini ni Shirikisho la soka nchini kuzuia usajili huo kuuingiza katika mfumo huku likigoma kumuondoa Kambole katika usajili huo likisema tayari lilishakamilisha mchakato wa kuwasajili wachezaji wa ndani na nje kwa timu zinazoshiriki michuano ya kimataifa.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Tayari shirikisho hilo la soka nchini limetoa maelekezo juu ya sakata hilo japo bado kwa upande wa Yanga sc mpaka sasa hawajatoa tamko lolote juu ya suala hilo.