Home Makala Kisinda Arudi Yanga sc

Kisinda Arudi Yanga sc

by Sports Leo
0 comments

Klabu ya Yanga sc imekamilisha usajili wa mshambuliaji wa pembeni Tuisila Kisinda kwa mkataba wa mkopo wa mwaka mmoja akitokea klabu ya Rs Berkane ya nchini Morroco ikiwa ni mwaka mmoja tangu aondoke klabuni hapo kujiunga na miamba hiyo ya Kaskasini mwa Afrika.

Kisinda alisajiliwa na Yanga sc msimu wa 2020/2021 kisha baada ya kutumika kwa mwaka mmoja alijiunga na klabu ya Rs Berkane baada ya kocha Florent Ibenge kumhitaji klabuni hapo ambapo ameisadia klabu hiyo kuchukua taji la kombe la shirikisho barani Afrika msimu uliopita.

Baada ya msimu kuisha na kocha Frolent Ibenge kuondoka klabuni hapo ndio ikawa mwisho wa Kisinda kusalia klabuni hapo baada ya kocha mpya kuonyesha kutompa kipaumbele na kuambiwa atafute timu ya kujiunga licha ya kwamba ana mkataba klabuni hapo.

banner

Tayari Yanga sc ilishakamilisha idadi ya wachezaji 12 wa kigeni kwa mujibu wa ligi kuu nchini lakini inasemekana kuwa Kisinda anachukua nafasi ya Lazarus Kambole ambaye amekua na majeraha ya mara kwa mara.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited