Kocha Mkuu wa West Ham United, David Moyes pamoja na wachezaji wawili wamekutwa na virusi vya Corona jana kabla ya kuanza raundi ya tatu ya mchezo wao wa Carabao Cup dhidi ya Hull.
Issa Diop na Josh Cullen ndio wachezaji waliokutwa na maambukizi ya Corona huku uongozi wa West Ham United ukithibitisha kwa taarifa hizo kuwa kwa sasa kocha huyo na wachezaji hao wapo chini ya uangalizi wa madaktari hadi afya zao zitakapokuwa salama.
Katika mchezo huo wa jana West Ham ilishinda kwa mabao 5-1 huku kocha msaidizi, Alan Irvine alichukua majukumu ya kukiongoza kikosi hicho kwa kipindi chote ambacho David Moyes atakuwa katika uangalizi.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.