Home Makala Kocha Simba sc Anaswa na Unga

Kocha Simba sc Anaswa na Unga

by Sports Leo
0 comments

Kocha wa makipa wa klabu ya Simba sc Muharami Mohamed amekamatwa na Mamlaka ya kuzuia na kupambana na dawa za kulevya sambamba na watuhumiwa wengine tisa akiwemo mmiliki wa akademi ya Cambiasso Sports ya jijini Dar es salaam Alhaj Kambi Zubeir.

Kipa huyo pamoja na wenzake hao wamekamatwa na kilo 34 za dawa za kulevya aina ya Heroin zenye Kilo 34.89 ambapo Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Tanzania (DCEA), Gerald Kusaya Kusaya amesema watuhumiwa wote wamekamatwa katika maeneo mbalimbali ndani ya nchi katika Operesheni iliyofanyika Oktoba, mwanzoni na Novemba 2022.

Kukamatwa kwa kipa huyo kumezua taharuki miongoni mwa waandishi wa habari na wadau wa soka nchini kutokana na jitihada kadhaa za kuongeza thamani mchezo wa soka nchini.

banner

Hata hivyo taarifa uliyotolewa na klabu ya Simba sc imemkana kocha huyo kuwa hakua mwajiriwa wa moja kwa moja wa klabu hiyo bali aliombwa kusaidia majukumu ya kuwanoa makipa wa kikosi hicho kwa kipindi hiki ambacho klabu hiyo inapambana kutafuta kocha mpya wa makipa.

Licha ya taarifa hiyo klabu ya Simba sc ilienda mbali zaidi kwa kuamua kumtambulisha kocha mpya wa makipa aitwae Chlouha Zakaria ambaye atungana na benchi la ufundi la klabu hiyo lililo chini ya kocha Juma Mgunda kwa sasa huku ikipanga mipango zaidi ya kuwatambulisha makocha wengine wawili.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited