Kocha wa zamani wa Yanga Sc, Mwinyi Zahera ametambulishwa rasmi Gwambina Fc kuwa kocha mkuu wa klabu hiyo ambayo imepanda daraja msimu huu wa 2019/20 na itashiriki ligi kuu bara msimu wa 2010/21.
Zahera amesaini dili la miaka mitano na tetesi zinaeleza kuwa ataanza kusajili nyota wake ambao alifanya nao kazi ndani ya Yanga.
Wachezaji wanaotajwa kuibukia Gwambina Fc ni Mrisho Ngasa na Kelvin Yondani ambao kwa sasa ni wachezaji huru ndani ya Yanga Sc baada ya mkataba wao kumalizika.