Mshambuliaji wa Liverpool anayefanya vizuri kimataifa na ni raia wa Senegal, Sadio Mane amekutwa na Virusi vya Corona baada ya kufanyiwa vipimo.
Liverpool imeweka wazi kuwepo kwa maambukizi hayo ya Virusi vya Corona kwa Mane licha ya kutoonysha dalili zozote na kwa sasa ametengwa maaalum chini ya uangalizi wa madaktari ili kuhakikisha anarudi kuwa na afya nzuri na kurejea uwanjani.
Mane anakuwa mchezaji wa pili Anfield kukutwa na Corona baada ya nyota wao mpya, Thiago Alcantara kukutwa naye ana Corona mapema mwanzoni mwa wiki hii.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Taarifa rasmi kutoka kwa mabingwa hao watetezi wa taji la ligi kuu England imesema kuwa kwa sasa wachezaji wake wote wanafuata taratibu zilizowekwa ili kurejea kwenye ubora wao na waendelee kwenye majukumu ya kupambania taji lao.