Home Makala Ligi Ya Marekani Kumvutia Suarez

Ligi Ya Marekani Kumvutia Suarez

by Sports Leo
0 comments

Virusi vya Corona vimeibua balaa kubwa katika klabu mbalimbali barani Ulaya ikiwemo Barcelona ambayo imepanga kuwapiga bei mastaa wake akiwemo Luis Suarez ili kujiingizia fedha ,hii ni kuutokana na La Liga kusimama ili watu wajikinge dhidi ya virusi hivyo vilivyoenea takribani dunia nzima.

Mmiliki wa klabu ya Inter Miami, David Beckham amenukuliwa akisema kuwa atafurahi kuona nyota huyo akitua kwao huku kwa upande mwingine klabu mbalimbali zinazoshiriki ligi kuu ya Marekani (MLS) zinatajwa kuwania saini ya nyota huyo.

Suarez mkataba wake ndani ya Barcelona unaenda hadi 2021 mbapo kuna kipengele cha kuongeza mwaka mmoja zaidi chenye masharti ya kucheza mechi kwa asilimia 60 msimu ujao.

banner

Nyota huyo alisema hivi karibuni hawezijua kama ataondoka Barcelona kwani bado ana mkataba nao ,lakini kwa mustakabali wa maisha ya baadaye anaona Ligi ya Marekani inamvutia sana pia ni sehemu nzuri.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited