Manchester United wamepoteza mchezo baada ya kuchapwa mabao 2-0 na Liverpool katika mchezo wa ligi kuu England uliochezwa katika uwanja wa liverpool kwa kusimamiwa na refa kutoka England Craig Pawson.
Mchezaji wa Manchester United Nemanja Matic alianza kwa kupewa kadi ya njano dakika ya 18 na dakika ya 14 bao la kwanza la Liverpool linapatikana kwa Virgil Van Dijik.
Dakika ya 25 David De Gea anapewa kadi ya njano pia Luke Shaw dakika ya 72 anapokea nae kadi ya njano wote wakiwa ni wachezaji wa Manchester United hii inamfanya kocha wao mkuu Ole Gunnar Solskjaer kunyong’onyea.
Mohamed Salah anakamilisha dakika 90 za mchezo kwa kuwapatia bao la pili timu yake ya Liverpool na anapokea pia kadi ya njano dakika ya tisini kabla ya kipenga kulia.
Liverpool inafikisha jumla ya pointi 64 ikiwa imecheza mechi 22 na kushinda mechi 21 ikiwa imetoka sare mara moja na kubaki kileleni kwa namba moja huku Manchester United ikiwa nafasi ya 5 ikiwa imecheza michezo 23 na kushinda michezo 9 huku ikiwa imetoka sare michezo 7 na kupoteza michezo 7 na kubaki na pointi 34.
Â
Â