Kiungo wa Simba Sc, Luis Miquissone leo Agosti 2,2020 amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa mchezo wa fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam.
Luis amehusika kwenye mabao yote mawili ya Simba akifunga bao la kwanza na kutoa pasi ya bao la pili kwa John Bocco katika mchezo wa leo dhidi ya Namungo Fc ambao wamechakazwa uwanjani kwa mabao 2-1 na kikosi hicho cha msimbazi.
Taji hili linakuwa la pili kwa Luis akiwa ndani ya Simba baada ya kuanza kutwaa taji la Ligi Kuu Bara na leo kupokea taji la Shirikisho.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.