Klabu ya Simba sc imemtambulisha rasmi Luís Miquissone kuwa mchezaji wao mpya baada ya kuondoka klabuni hapo takribani misimu miwili iliyopita na kwenda kujiunga na Al Ahly ya nchini Misri.
Simba sc imemrejesha mchezaji huyo kwa kuamua kumpa mkataba wa miaka mitatu akiwa kama mchezaji huru baada ya kufanikiwa kuvunja mkataba wake na klabu ya Al Ahly kwa makubaliano ya pande mbili.
Luís Miquissone tangu asajiliwe na mabingwa hao wa Afrika amekua akitolewa kwa mkopo mara kadhaa hasa baada ya kukosa namba katika kikosi cha kwanza tangu aondoke kocha Pitso Mosimame ambaye alimsajili.
Mchezaji huyo tayari yupo nchini akishughulikia taratibu za safari ili ajiunge na kambi ya timu hiyo nchini Uturuki kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya wa ligi kuu na michuano ya kimataifa ambapo Simba sc itashiriki michuano maalumu ya Super League.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Simba sc imekua na misuli ya usajili za gharama msimu huu hasa baada ya kupata takribani bilioni 5 za maandalizi ya michuano hiyo.