Home Makala Makonda Kuipa Nguvu Stars Misri

Makonda Kuipa Nguvu Stars Misri

by Sports Leo
0 comments

Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paulo Makonda amewasili nchini Misri kwenda kuipa hamasa timu ya taifa ya Tanzania kufuatia kupoteza mechi ya awali dhidi ya Senegali kwa mabao mawili kwa bila.

Makonda amewasili nchini humo kufuatia kukubaliwa ombi lake la kwenda nchini humo na Raisi Magufuli hapo jana wakati akizindua gesi (Taifagas) kurasini jijini Dar es salaam ambapo mkuu huyo wa mkoa wa Dar es salaam alipewa ruhusa maalumu na Raisi ili kuhakikisha timu hiyo inaibuka na ushindi kwenye mechi zilizosalia dhidi ya Kenya na Algeria.

Taifa Stars imebakiwa na mechi mbili baada ya kupoteza mchezo wa kwanza dhidi ya senegali na kesho usiku itashuka dimbani kutafuta alama tatu dhidi ya majirani wa Kenya anayoichezea kiungo Victor Wanyama wa Tottenham Hotspurs.

banner

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited