Manchester United imekamilisha usajili wa mchezaji Donny van de Beek kwa ada ya Paundi Milioni 40 ambayo inaelezwa kuwa atalipwa paundi 107,000 kwa wiki.
Van de Beek amesaini kandarasi ya miaka mitano ndani ya mashetani hao wekundu akitokea klabu ya Ajax ya Uholanzi huku akipewa jezi namba 34.
Usajili huu unakuwa wa kwanza kwa Kocha Ole Gunnar Solskjaer katika usajili wa 2020/2021 ambapo Van de Beek anatarajiwa kutengeneza muunganiko mzuri katika nafasi ya kiungo akishirikiana na Paul Pogba pamoja na Bruno Fernandes.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.