Manchester United imekamilisha usajili wa beki Aaron Wan-Bissaka kutoka klabu ya Crystal Palace kwa kiasi cha paundi 50m bei ambayo imemfanya beki huyo kuwa beki wa pembeni ghali zaidi kwa sasa.
Wan-Bissaka amesajiliwa baada ya majadiliano ya muda mrefu baina ya timu hizo mbili hasa kuhusu dau la usajili japo mchezaji huyo alishakubaliana na man united mshahara wa paundi elfu 80 kwa wiki.
Beki huyo anayeichezea timu ya vijana ya Uingereza chini ya miaka 21 ni zao la akademia ya timu hiyo na alipandishwa timu ya wakubwa na kufanikiwa kucheza michezo 46 tu iliyomfanya kuchaguliwa kuwa mchezaji bora wa klabu hiyo kwa msimu huu wa ligi ulioisha.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Bissaka atatambulishwa rasmi leo hii ijumaa kwa mujibu wa taarifa za ndani ya klabu hiyo baada ya kuwa jijini manchester kwa ajili ya kukamilisha taratibu za kujiunga na klabu hiyo ikiwemo kufanyiwa vipimo vya afya.