Manchester wamejizolea ushindi wa mabao 4-0 kutoka kwa Norwich City mchezo uliochezwa jana uwanja wa Old Traford.
Mabao mawili yalifungwa na Marcus Rashford la kwanza dakika ya 22 na bao la pili dakika ya 52 kwa njia penalti.
Antony Martial aliongeza bao la tatu dakika ya 53 na Mason Greenwood akamaliza siku nzuri kwa mashetani wekundu dakika ya 78.
Manchester imefikia jumla ya pointi 34 ikiwa nafasi ya tano huku Norwich ikibaki na pointi zake 14 ikiburuza mkia kwenye nafasi ya 20.
Ulikuwa ushindi mzuri kwa wachezaji wa Reds na Ole Gunnar Solsjaer alifurahi kuwa na washambuliaji wenye malengo ya kujiimarisha.
Â