Home Makala Mane Kuikosa Kombe la Dunia

Mane Kuikosa Kombe la Dunia

by Sports Leo
0 comments

Sadio Mane wa Senegal yupo hatihati ya kukosa fainali za kombe la Dunia zitakazofanyika nchini Quatar mwezi huu baada ya kuumia sehemu ya mguu wake katika mchezo baina ya klabu yake ya Bayern Munichen dhidi ya Werder Bremen uliofanyika usiku wa jumanne Novemba 8.

Katika mchezo ambao Bayern waliibuka na ushindi wa mabao 6-1 Mane alilazimika kutolewa dakika ya 15 ya mchezo na nafasi yake kuchukuliwa na Leroy Sane ambapo leo ndio imetoka taarifa kwamba jeraha hilo linahitaji uchunguzi zaidi wa kitaalamu ili kumtibu baada ya kujua ukubwa wake na kuacha wasiwasi huenda akawa hajapona mpaka fainali zinaanza.

Mane ni muhimu katika kikosi cha Senegal ambapo aliwasaidia kuchukua ubingwa wa michuano ya kombe la mataifa ya Afrika mwaka huu na tayari vyanzo vya kuaminika ikiwemo gazeti la L’EQUIPE imeripoti kuwa atakosa fainali hizo kubwa duniani japo Kocha wake Julian Nagelsmann hakuthibitisha hilo.

banner

Kocha Alliou Cisse anatarajiwa kutangaza kikosi cha wachezaji 26 watakaoiwakilisha nchini hiyo ya Senegal katika fainali za kombe la dunia mwaka huu nchini Quatar.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited