Hatimaye baada ya tetesi za muda mrefu sasa rasmi kipa Aishi Manula Arejea Azam Fc baada ya kuwa amemaliza mkataba wake wa miaka miwili na klabu ya Simba Sc aliousaini misimu miwili iliyopita.
Azam Fc imemsajili Manula kwa mkataba wa miaka mitatu ambapo imemtambulisha rasmi tayari kabisa kujiandaa na msimu ujao wa ligi kuu ambapo sasa timu hiyo itakua chini ya kocha Frolent Ibenge kama kocha mkuu wa klabu hiyo.
Manula sio mgeni katika viunga vya Chamazi Complex ambapo alikua hapo mpaka mwaka 2017 alipoondoka na kujiunga na Simba sc ambapo amekaa kwa miaka nane kama kipa namba moja wa klabu hiyo akiisaidia katika michuano mbalimbali kumaliza nafasi za juu.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Hata hivyo mahusiano baina ya Manula na Simba sc yaliingia dosari baada ya kipa huyo kuruhusu mabao matano katika kipigo cha 5-1 ilichokipata Simba Sc kutoka kwa Yanga sc katika ligi kuu machi 20 2024 hali iliyopelekea kuonekana kama alikula rushwa madai ambayo hayajathibitishwa mpaka leo.
Tangu hapo amekua akikaa jukwaani na mara chache amekaa benchi kutokana na kipa Moussa Camara kuwa chaguo la kwanza klabuni hapo huku akisaidia na kipa Ally Salim mara kwa mara.