Baada ya danadana kuhusu lini watawasili nchini hatimaye msafara wa timu ya Marumo Gallant ya nchini Afrika kusini umefanikiwa kuwasili nchini alfajiri ya leo katika uwanja wa Mwl.Julius Nyerere jijini Dar es salaam.
Mara baada ya kuwasili msafara wa timu hiyo uligomea kupanda basi la lililoandaliwa na wenyeji wao Yanga sc na kupanda basi jingine ambalo wamelitafuta wenyewe na kuelekea hotelini moja kwa moja.
Timu hizo zitakutana kesho katika mchezo wa nusu fainali ya kombe la shirikisho unaotarajiwa kuanza majira ya saa kumi za jioni katika uwanja wa Benjamini Mkapa ambapo watarudiana tarehe 17 Mei mwaka huu.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.