Msemaji wa Ruvu Shooting Masau Bwire amekiri kuwa aliwahi kuvishabikia vilabu vikongwe hapa nchini vya Simba na Yanga alipokuwa kijana mdogo kabla ya kuamua kuzikacha timu hizo kwasababu tofauti tofauti.
Masau ameyasema hayo alipokuwa akijibu maswali ya watangazajin wa kipindi cha leo tena kinachorushwa na kituo cha clouds fm hii leo alipokuwa akifanya promo ya tamasha la klabu yake ya Ruvu litakalofanyika kesho mkoani Pwani.
Katika kujibu swali kuwa yeye ni shabiki wa timu gani kati ya hizo mbili,yeye alijibu kwa kusema kuwa ni kweli alizishabikia timu hizo alipokuwa mdogo alkini si kwasasa kwani hana tena mapenzi na timu hizo.
Bwire alisema kuwa alianza kuishabikia Simba kutokana na msukumo wa kaka yake aliyekuwa anaipenda sana timu hiyo,aliendelea kwa kusema kuwa siku moja kaka yake huyo alibandika magazeti yenye picha za wachezaji wa Simba,na yeye aliamua kutoboa macho ya wachezaji waliokuwa kwenye picha hiyo ambapo kulimpelekea kaka yake kupa kipigo cha maana kilichomfany tangu siku hiyo kuichukia Simba na kuhamia kwa watani wao Yanga.
Sababu iliyompelekea Masau Bwire aichukie pia Yanga ni kipigo kutoka kwa mwalimu wake wa hesabu aliyempa bakora za maana baada ya kutohudhiuria shule kutokana na uwepo wa mechi ya watani wa jadi kwa vijana wa kijijini kwao,Masau hakwenda shule siku hiyuo ili akacheze mechi hiyo kabla ya kesho yake kufikwa na madhira hayo.
Tangu kipindi hicho anasema alivichukuia vilabu hivyo kwani vilikuwa vinamsababishia vipigo kila mara.
Masau pia anasema kuwa alishawahi kupewa ofa na vilabu hivyo pamoja na Azam FC kuwa msemaji lakini aliamua kubaki zake Ruvu Shooting ambayo inampa amani anapoitumikia.
Ruvu Shooting wamekuja na tamasha lao la usiku wa Ruvu ambalo ni maalumu kwa ajili ya kuisogeza timu hiyo karibu zaidi na wakazi wa Pwani,pia watazindua jezi mpya,kutambulisha wachezaji pamoja na mechi za kirafiki huku tukio zima likirushwa mubashara na azamtv.
Msemaji huyo kipenzi cha mashabiki wengi wa soka nchini amejizolea umaarufu mkubwa kutokana na misemo yake inayoleta burudani kama vile papasa,tikisa akitumia kama kuwacharua wapinzani wa Ruvu Shooting kwenye mechi mbalimbali.Pia ameweka wazi kuwa malengo yao ni kuchukua ubingwa wa ligi kuu au kupata nafasi ya kuiwakilisha nchi katika mashindani ya kimataifa.