Home Makala Mashabiki Elfu 60 Kuiona Simba sc

Mashabiki Elfu 60 Kuiona Simba sc

by Sports Leo
0 comments

Shirikisho la soka barani Afrika(Caf) limeiruhusu klabu ya Simba sc kuingiza mashabiki elfu 60 katika mchezo wa hatua ya robo fainali ya kombe la shirikisho barani Afrika utakaofanyika April 17 katika uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.

Simba sc iliomba kwa shirikisho hilo kuruhusiwa kuingiza mashabiki wengi kadri ya uwezo wa uwanja wa Benjamin Mkapa ambapo baada ya Caf kujiridhisha kuhusu uimara wa Simba sc katika kusimamia usalama wa mashabiki viwanjani hasa katika kipindi hiki cha ugonjwa wa Uviko 19 limeamua kuruhusu idadi hiyo ya mashabiki.

Awali klabu hiyo haijawahi kuruhusiwa kuingiza idadi ya mashabiki wengi kiasi hiki ambapo mara nyingi iliruhusiwa mashabiki takribani wasiozidi elfu 35 pekee.

banner

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited