Home Makala Masoud Djuma Atupiwa Virago

Masoud Djuma Atupiwa Virago

by Sports Leo
0 comments

Kocha Masoud Djuma ametimuliwa katika klabu ya Dodoma Jiji Fc baada ya kuwa na mfululizo wa matokeo yasiyoridhisha katika ligi kuu nchini ikishinda mchezo mmoja pekee na kutoa sare michezo miwili huku ikifungwa michezo mitatu katika michezo sita ya ligi kuu nchini.

Wengine waliotupiwa  virago ni pamoja na kocha msaidizi Mohammed Muya,Kocha wa makipa Adam Meja ambaye inadaiwa amejiunga na Simba Queens ambapo kutokana na kuwa na matokeo yasiyoridhisha imeifanya timu hiyo kusalia mwishoni mwa msimamo ambapo inashika nafasi ya 14.

Taarifa iliyotolewa mapema hivi leo inasema kwamba Djuma ametimuliwa sambamba na wasaidizi wake ili kutoa nafasi ya kuunda benchi jipya la ufundi kuhakikisha kuwa kikosi hicho kinarudisha makali yake .

“Uongozi wa klabu unawashukuru kocha mkuu pamoja na benchi lote la ufundi kwa mchango wao mkubwa ndani ya klabu yetu na inawatakia kila heri katika majukumu yao mapya,”ilieleza taarifa hiyo.

Kocha huyo ambaye aliwahi kuwa kocha msaidizi wa klabu ya Simba sc anaondoka klabuni hapo baada ya kudumu kwa takribani miezi nane tangu atambulishwe mwezi februari mwaka huu na sasa kikosi kitakua kwa muda chini ya kocha wa timu ya vijana Omary Mohammed mpaka pale atakapopatikana kocha mpya.

 

 

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited